6 Desemba 2012 - 20:30

Saudia Arabia,Kuweit na baadhi ya nchi za kiarabu ziekuwa zikifurahia vikwazo dhidi ya Jamhuri ya kiislam ya Iran na kujipendekeza kwa Marekani na vibaraka wake na kumba kuwa Iran idhibitiwe mapema hofu yao kubwa ni kuenea fikra za utala wa Jamhuri ya kiislam ya Iran katika nchi zao na tofauti za Shia na Sunni.

chuki ya baadhi ya nchi za kiarabu dhidi ya Jamhuri ya kiislam ya Iran hasa mataifa ya kiirabu yaliyokaatika ghuba ya Uajemi inatokana na maendeleo ya Iran yanayoonekana kukua kwa kasi na kutabirika kuwa punde si punde Iran itatawala sehemu kubwa ya eneo la ghuba ya Uajemi na mashariki ya kati kwa jumla.hofu hiyo ya maendeleo ya Jamhuri ya kiislam ya Iran imevishwa nguo ya vita dhidi ya Silaha za maangamizi(Nyuklia) na vita dhidi ya ushia wakidhani kuwa jamhuri ya kiislam ya iran kwa kuwa ni Jamhuri ya kiislam iliyochini ya madhehebu ya Shia  basi inafaa kupigwa  vita kwa hali na mali ilihali wanafumbia macho kuwa ingawa iran si taifa la kiiarabu ni taifa la kiislamhiyo yawapasa kuangalia kuwa wairan ni waislam wenzaona si kuangalia kuwa ni waarabu wenzao au la! fauka ya hayo Iran imekuwa ikiwasaidia waarabu mfano imekuwa ikiwasaidia Syria,Lebanon na Parestina bila kujali kuwa inasaidia waarabu au inasaidia masunni bali Jamhuri ya kiislam ya Iran inatazama kuwa inasaidia waislam wasimalizwe na njama za maadui wa Uislam ambao kwa bahati mbaya kwa sasa nchi za kiarabu ziko bega kwa beda na maadui wa uislam wakishambulia mataifa ya kiislam.