17 Januari 2013 - 20:30

Dr. Sayyid Tijani Al-Samawi Mshia maarufu wengi watambua kuingia kwake katika Madhehebu ya Ahlul Bayt(as), Dr. kapata taufiki ya kutumikia na kusafisha Haram ya Imam Husein(as).

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Dr. Sayyid Tijani Al-Samawi Mshia maarufu wengi wafahamu kisa cha kuchagua kwake Madhehebu ya Ahlul Bayt(as), Mwaka huu alipata taufiki ya kusafisha Haram ya Imam Husein(as) Karbala na kuwa mmoja wa wafanyakazi wa Imam Husein(as).

Mwandishi maarufu Dr. Sayyid Tijani Al-Samawi alipata taufiki hiyo baada tu ya kuhudhuria katika ziara ya Imam Husein(as) Karbala.

Asili ya Dr. Sayyid Tijani Al-Samawi ni Iraq na nasaba yake ya rejea katika ukoo mkubwa Al-Samawi nchini Iraq ambapo baadhi ya mababu zake walihama kwenda Tunisia katika Bara la Afrika.

Dr. Sayyid Tijani Al-Samawi alizaliwa tarehe 2/2/1943 katika Mkoa wa Qudhah kusini mwa nchi ya Tunisia, Na alisoma katika Shule za msingi za Wafaransa zilizokuepo Tunisia na kupata Shahada ya hali ya Juu katika Tahasusi za Falsafa na Elimu ya Mwanadamu, Aidha alipofikisha miaka 10 alihifadhi nusu ya Qurani Tukufu.

Dr.Tijani katika safari zake za Bairut alikutana na Bw. Mun`im ambaye alikuwa Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Iraq na Mwalimu huyo alikua katika Madhehebu ya Ahlul Bayt(as), Na baada ya kupata taathira ya Madhehebu ya Ahlul Bayt(as) alisafiri kuelekea Najaf kuonana na Ayatullah khui ili kufahamu zaidi Madhehebu yaho vizuri.

Sheikh Tijani Al-Samawi hadi sasa amikwishatunga Vitabu 11 miongoni mwavyo ni; ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI, HATIMAE NIONGOKA, MASHIA NDIO MASUNNI.

Dr. Tijani Al-Samawi ni miongoni mwa Wanajumuiya wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as) na alishiriki katika Mkutano wa wiki ya Ghadir ulofanyika Tehran mwaka huu.