27 Januari 2013 - 20:30

Vyanzo vya habari nchini Misri vyanukuu kuruhusiwa Jeshi la nchi hiyo kukamata wafanya vurugu na wavunjishaji amani nchini humo

Shirika la habari la  AhlulBayt(a.s)-ABNA: Televishen ya Al Arabia imetangaza kuwa bunge la Misri limetoa ruhusa ya kukamatwa wananchi wanaoleta vurugu nchini humo.Kwaupande mwengine mkuu wa mahakama ya Misri ametoa taarifa ya kufuatilia matukio na vurugu zinazotokea baina ya wananchi na jeshi la polisi katika miji tofauti nchini humo. Naye katika ukurasa wake wa Fecebook ameandika kuwa jeshi la ulinzi limefanikiwa kuwashika watu 77  kati ya waleta fujo hiyo ambapo watu 6 kati yao wamehukumiwa kifungo na uhakiki unaendelea kunako watu 71 waliobaki.Katika vurugu hizo zinazoendelea katika viwanja vya Tahriri mpaka sasa mtu mmoja amefariki katika furugu hizo, kwamujibu wa taarifa hizi mpaka sasa vurugu hizo zinaendelea katika s daraja la Qasri Nil baina ya jeshi la polisi na wananchi nakupelekea jeshi hilo kutumia mabomo ya machozi hasa baada ya kumaliza  sala ya dhuhuri.