Mtoto alipozaliwa alizaliwa katika kivuli cha Mwenyezi Mungu na kumtabua muumba wake, baada tu ya kuja duniani mazingira, Baba, Mama na ndugu zake ndio humbalisha muelekeo wake, pamoja ya kuwa Mtoto amezingirwa na fikira tofauti za kukubalia au kukataa Muumba wa mbingu na ardhi; ni lazima kwa Baba na Mama kutumia fursa yao kumfunza jinsi ya kujiuliza na kumfahamu muumba wake na kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu yupo kulingana na upeo wake wa kifikra, maneno haya ni ya Maulamaa na Wanazuoni wakididi na Maulamaa wa Elimu ya Nafsi (Saikolojia).
Malezi na mafunzo ya Mtoto lazima yawe kwa daraja kulingana na umri wa Mtoto unavyokuwa, daraja ya kukuwa Mtoto kilugha na kiakili imefupishwa na kubainishwa na Imam Muhammad Baqir(as) akisema: ATAKAPOFIKIA MTOTO MIAKA MITATU AAMIBIWE: SEMA LAA ILAAHA ILLA LLAH MARA SABA, KISHA AACHIWE MPAKA ATAKAPOFIKISHA MIAKA MITATU NA MIEZI SABA NA SIKU ISHIRINI AAMBIWE: SEMA MUHMMADUN RASULULLAH MARA SABA, KISHA AACHIWE MPAKA ATAKAPOFIKISHA MIAKA MINNE AAMBIWE: SEMA ALLAHUMMA SALI ALAA MUHAMMAD WA AALI MUHAMMAD MARA SABA, KISHA AACHIWE MPAKA ATAKAPOFIKISHA MIAKA MITANO AAMBIWE NA KUULIZWA MKONO WAKO WA KULIA NI UPI NA WA KUSHOTO NI UPI? ATAKAPO FAHAMU AELEKEZWE KIBLA NA AAMBIWE: SUJUDU, KISHA AACHIWE MPAKA ATAKAPOFIKISHA MIAKA SABA, KISHA ATAKAPOFIKISHA MIAKA BASA AAMBIWE OSHA USO WAKO NA VIGANJA VYAKO, AKIOSHA AAMBIWE: SWALI, KISHA AACHIWE MPAKA ATAKAPOFIKISHA MIAKA TISA, NA ATAKAPOFIKISHA MIAKA TISA AFUNDISHWE KUTAWADHA NA KUPIGWA KWA AJILI YA UDHUU NA AAMRISHWE KUSWALI NA APIGWE KWA AJILI YA SWALA NA AKIFAHAMU KUTAWADHA NA KUSWALI MWENYEZI MUNGU AMSAMEHE YEYE NA WAZAZI WAKE INSHAALLAH.
Haya ndio mafunzo sahihi ya kiislamu kwa watoto kumtabua Mwenyezi Mungu, Uislamu ni Dini ilokamilika katika kila nyanja, Mtume Mtukufu Muhammad(s.a.w.w) na Ahlul Bayt zake(as) walikwisha weka wazi kila aina ya mafunzo ya jamii, kwa hiyo jamii kama yataka kuongoka lazima ishikane watu hawa kwa kutaka muongozo wao wa dunia na akhera hasa muongozo wa jamii hii tuliyokuemo ambayo ni njia tu na maandalizi ya maisha ya milele.
Na Khamis Sadik