Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa tume hiyo Isaack Hassan amesema Kenyatta ambaye ni mtoto wa muasisi wa nchi hiyo, ameshinda uchaguzi huo wa 10 tangu nchi hiyo ijipatie uhuru. Amesema Kenyatta amepata asilimia 25 ya kura katika majimbo 32 kati ya 47, ambazo ndizo zinazohitajika ili kuepuka kurejewa kwa uchaguzi.
9 Machi 2013 - 20:30
Msimbo wa Habari: 398469
Tume ya uchaguzi ya Kenya leo imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa rais wa Jamhuri ya Kenya baada ya kupata kura milioni 6.17 na kumshinda mpinzani wake Raila Odinga.