Shirika la habari la AhlulBayt(a.s) ABNA; Rais wa shirika la mafuta nchini Libya ameema; hofu ya mashirika ya mafuta ya nchi za nje kutokana na baadhi ya vurugu zinazotokea katika nchi hiyo haitapelekea Libya kutuwa ruhusa ya majeshi ya nje kuingia katika nchi hiyo kwa kusingizia kulinda amani na kuhifadhi visima vya mafuta vya nchi hiy.Naye katika maelezo yake alisisitiza kuwa kamwe haitatolewa ruhusa hiyo kwa majeshi hayo kuwepo katika taasisi za mafuta.Aliyasema hayo katika mkutano uliofanyika baina yake na msafara wa shirika la mafuta la Wingereza uliofanyika katika mji mkuu wa nchi ambapo mkutano huo ulikuwa kwaajili ya uchunguzi kuhusu ulinzi na usimamizi wa sehemu za mafuta nchini Libya.Shirika la mafuta la Wingereza baada ya kutokea tukio la kigaidi katika taasisi ya Gesi nchini humo, lilitangaza kuchunguza zaidi kunako ratiba zake za kuchimba visima vya mafuta nchini humo.Libya toka kupinduliwa utawala wa Gadafi mpaka sasa ni miezi 18 utawala mpya wa nchi hiyo mpaka sasa hujaweza kusimamia suala la ulinzi wa nchi nzima.
11 Aprili 2013 - 19:30
Msimbo wa Habari: 408472
Serikali ya Libya imeisitiza kuwa daima haitatoa ruhusa kwa majeshi ya nje kuwepo katika nchi hiyo kwa kusingizia kulinda amani