18 Juni 2013 - 19:30
Misri:  hatuna mfungwa wa kisiasa

Msaidzi wa waziri wa masuala ya wafungwa nchini Misr katika kuashiria hatua ya uangalizi wa amani walio chukua kwaajili ya kuwasaidia wafungwa wa nchi hiyo ameahidi kuto kujirudia matukio ya kuvamiwa kwa jela za nchi hiyo kama ilivyotokea kipindi cha mapinduzi nchini humo

Shirika la habari la AhlulBayt(a.s)- ABNA; “Mustafa Bazi” msaidizi wa waziri wa masuala ya jela na wafungwa nchini Misri amesema; usimamizi na ulinzi wa amani katika jela za Tarah, wadi Natruni na Burjil Arab ukochini ya jeshi la ulinzi la  nchi hiyo.Naye aliongeza kusema kuwa usimamizi maalumu kwaajili ya ulinzi wa jela hizo za Misri kutokana na  matukio yaliotokea katika kipindi cha mapinduzi katika jela hizo na kuhakikisha kuwa matukio hayo hayata jikariri tena nchini humo.Msaidizi wa waziri huyo amefafanua kuwa; sisi tuna matumaini makubwa na wananchi wa Misri  na tunayakini kuwa kutokana na matukio na mazingira magumu ya kusikitisha yaliotokea katika nchi hiyo kipindi mapinduzi kamwe hatuta toa mwanya wa kujitokeza matukio kama hayo nchini Misri.Naye amesema; kipindi cha mapinduzi ya nchi hiyo januari 25 wafungwa elfu 24 walikimbia na kutoroka katika jela hizo ambapo wafungwa elfu kumi na mbili na miatatu wamefanikiwa kukamatwa kwa mara nyengine na hivi sasa mahakama ya nchi hiyo inachunguza chanzo kilicho sababisha kukimbia na kutoroka wafungwa hao.Mustafa Bazi amebainisha: katika jela hizo zote hatuna mfungwa yoyote wa masuala ya kisiasa.Hii ni katika hali ambayo viongozi wa jeshi katika mkoa Alqulyubiyah nchini Misri wamatangaza kuwa siku ya tarehe 30 juni hatutajihusisha na suala lolote na tutabaki katika sehemu zetu za ulinzi kwani tumejifunza katika matukio yaliopita (Inasemekana kuwa 30/6/2013 kutafnya maandamano makubwa dhidi ya serikali ya Misri) nao wamesisitiza kuzilinda sehemu za kazi zao hata kama itatugharimu maisha yetu.