18 Julai 2013 - 19:30
Marekani yafeli nchini Lebanon

Lebanon yauomba Umoja wa Ulaya usikiweke chama cha Hizballah kwenye orodha ya makundi ya ugaidi

Ripoti ya ABNA Serikali ya Lebanon imeuomba Umoja wa Ulaya usiweke chama cha Hizballah cha Lebanon kwenye orodha ya makundi ya ugaidi, na kuutaka Umoja huo usitoe uamuzi bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha.

Katika taarifa iliyotolewa na serikali ya Lebanon jana, serikali hiyo imesema, chama cha Hizballah ni sehemu muhimu ya jamii ya Lebanon, na kinaungwa mkono na waislam wengi wa dhehebu la Shia, na kina viti katika serikali ya Lebanon na bunge la nchi hiyo.