Ripoti ya ABNA- Habari kutoka televisheni ya taifa ya Misri zinasema, kutokana na suala la usalama, chama cha Muslim Brotherhood kimefuta maandamano mengi yaliyopangwa kufanyika tarehe 18 huko Cairo. Takwimu kutoka serikali ya Misri zimeonesha kuwa operesheni ya kuwafukuza waandamanaji iliyofanyika tarehe 14, na mapambano yaliyotokea baada ya hapo kote nchini humo Misri yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 866.Waziri mkuu wa Iraq Bw. Nuri al-Maliki ametoa taarifa akisema, anaunga mkono hatua iliyochukuliwa na serikali ya mpito ya Misri dhidi ya waandamanaji wanaomuunga mkono Bw. Mohamed Morsi ili kulinda utulivu wa nchi.
18 Agosti 2013 - 19:30
Msimbo wa Habari: 453328
Naibu waziri mkuu wa kwanza wa Misri ambaye pia ni waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Bw. Abdel Fatah al-Sisi amesema, jeshi la Misri siku zote litalinda uhuru wa wananchi wa kuchagua kiongozi kutokana na matakwa yao. Amesema jeshi la nchi hiyo kamwe halitavumilia kitendo chochote cha kuharibu usalama wa nchi, watu wanaodhani kuwa wataweza kuivuruga Misri na wananchi wake kwa kutumia nguvu, wanapaswa kujikosoa.