Shirika hilo ni mamlaka ya utekelezaji wa mkataba wa kupiga marufuku silaha za kemikali.
Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky, katibu mkuu wa umoja huo Ban Ki-moon amepata ombi la Syria la kujiunga na mkataba wa kupiga marufuku silaha za kemikali, na nchi hiyo itasaini rasmi mkataba huo baada ya siku 30, yaani Oktoba 14, ambapo mkataba huo utaanza kufanya kazi kwa nchi hiyo.