ongozi Muadhamu wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran Sayyid Ali Khamenei pamoja na viongozi wa Serikali ya Iran ameungana na mamilioni ya wapenzi wa bwana mtume Muhammad s.a.w katika kuadhimisha tukio la Ashuraa, ambalo ni tukio la kutisha zaidi katika matukio yaliyowahi kutokea katika historia ya wanadamu, kwani miaka 1400 iliyopita Imam Husein a.s mjukuu na kipenzi cha mtume Muhammad s.a.w aliuawa kikatili yeye na familia yake nakisha kukatwa vichwa vyao.Mashia na wapenzi wa mtume Muhammad duniani kote wamekuwa wakuomboleza masiku haya ya msiba mkubwa na jinai zilizofanywa na utawala wa Yazid bin Muawiyah ambaye ni moja kati ya watawala katili waliochukua madaraka ya uislamu kwa mabavu.Shirika la Habari la Ahlul Bayt linatoa mkono wa Tanzia kwa wapenzi na wafuasi wa familia ya mtume Muhammad s.a.w


12 Novemba 2013 - 20:30
Msimbo wa Habari: 480663
Kiongozi Muadhamu wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran Sayyid Ali Khamenei pamoja na viongozi wa Serikali ya Iran ameungana na mamilioni ya wapenzi wa bwana mtume Muhammad s.a.w katika kuadhimisha tukio la Ashuraa .