14 Novemba 2013 - 20:30
Muhammad Mursiy aamishiwa jela ya mtu mmoja

Mmoja kati ya viongozi wa Misri atoa habari yakuwa Muhammad Mursiy, Rais wa jamhuri ya Misri aliye enguliwa hivi punde kuamishiwa katika jela ya pekee iliopo mkoa wa Iskandaria nchini Misri katika Burjil Arab

Shirika la habari la AhlulBayt (a.s)- ABNA; msaidizi wa kwanza wa waziri wa mambo ya ndani nchini Misri (Ahmad Hilmiy) amesema; viongozi wa ulinzi nchini humo wamtuhumu Rais huyo kwa kuuwa waandamanaji nchini humo, na mpaka sasa rais huyo bado yuko jela na sasa wameamua kumuamishia katika jela ya pekee iliopo katika jingo la Burjil Arab katika mkoa wa Iskandaria.Masaidizi huyo aliendelea kusema; Muhammad Mursiy kutokana na hali yake ya kimwili kuwa sinzuri alitoliwa nje kwa muda wa siku 10 na muda huo aliokuwa amepewa umesha kwisha.Baadhi ya vyanzo wa ulinzi wamenukuu kuwa kuwekwa kwa Rais huyo katika jela ya pekee ni kwakele walichokidai kuwa viongozi wa jela hizo kukhofia usalama wake kutokana na wafungwa wengine wasimdhuru.Mahakama ya jinai mjini Cairo imeamua kusitisha kusikiliza hukumu ya faili la Rais huyo na wenzake wengine 14 ambao wanahusika katika tuhuma ya kuuwa waandamanaji nchini humo na badara yake  kupangwa mnamo tarehe 8 mwezi wa kwanza mwaka ujao.