Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ANBA: maonyesho hayo yalifanyika kwa kushirikiana na kituo cha mafunzo ya lugha ya kifarsi katika mkoa wa Ladhikiyah ilioko chini ya makao makuu ya kituo cha utamaduni wa Iran nchini Syria.
Maonyesho hayo zilionyeshwa athari za mpiga picha wa Syria mheshimiwa “Nibrasi Ally” iliokuwa na anuani ya “mtazamo kuhusu maendeleo ya serikali ya kiislamu ya Iran” yaliofanyika tarehe 10 mwezi huu nchini Syria.
Katika maonyesho hayo kulionyeshwa picha mbali mbali zinazoashiria maendeleo ya jJamhuri ya kiislamu ya Iran katika Nyanja tofauti kama ujenzi, viwanda, sanaa na masuala mengine ya kitekinolojia ya Iran, pia zilionyshwa picha zinazoonyesha fungamano la kijamii baina ya Iran na Syria.
Pia katika maonyesho hayo ilionyeshwa picha ya nyumba ya mwazilishi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran Imam Khumain iliopo Jamarani katika mji mkuu wa Iran Tehran.
Maonyesho hayo yalihudhuriwa na watu wengi ambao ni wakazi wa Syria takriba ni zaidi ya watu 1000, na katika masiku ya mwisho ya maonyesho hayo kwaniaba ya wananchi muingiza mmoja maarufu nchini humo alitoa shukurani kwa kituo cha mafunzo ya Lugha ya kifarsi katika mkoa huo nakuishukuru Jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa misaada yake kwa wananchi wa Syria.
Rejea: ABNA
14 Mei 2014 - 20:24
Msimbo wa Habari: 608621
Maonyesho yenye anuani ya “maendeleo ya Jamhuri ya kiislam ya Iran” yamefanyika katika makao makuu ya kituo cha utamaduni wa Iran katika manispaa ya Jiblah mkoani Ladhikiyah nchini Syria