Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Muhammad Rahisa mmoja kati ya wakuu wa kikundi cha waasi hao alipokuwa akizungumza kwa simu na mwandishi wa Habari wa Ufaransa alisema: sisi hivi sasa tumeuteka mkowa wa Kidal katika kila pande, pia tunaidadi kadha ya mateka tuliowateka katika mpambano haya ambapo asilimia kubwa kati yao ni wanajeshi.
Hii ni katika hali ambayo mmoja kati ya viongozi wa jumuiya ya umoja wa mataifa amesema, katika mahojiano na waandishi wa habari wa Ufaransa, alisisitiza kuwawa kwa idadi kadhaa ya wanajeshi wa Mali na kutekwa baadhi ya wengine mioungoni mwao.
Baada ya kutekwa mkoa huo na waasi hao jeshi la taifa hilo limenaza kupambana vikali na waasi hao kwaajili ya kuukomboa mkoa huo, mwandishi wa ufaransa akinukuu kutoka kwa walioshuhudia tukio hilo alitangaza kuwa mapambano yanaendelea katika sehemu hiyo baina ya jeshi la nchi hiyo na waasi hao katika ineo hilo la kaskazini mwa mashariki mwa Mali.
Rejea: IRNA
21 Mei 2014 - 20:43
Msimbo wa Habari: 610400
Waasi nchini Mali wauteka mkoa wa Kidal kaskazini mwa mashariki mwa nchi hiyo ambapo waliuteka siku ya jumanne baada ya mapigano makali yaliotokea baina yao na jeshi la nchi hiyo