22 Mei 2014 - 15:28
Hofu ya wizi wa kura Malawi

Rais wa Malawi Bi Joyce Banda ameelezea hofu yake kuhusu kutokea udanganyifu na wizi wa kura za uchaguzi wa kinyang'anyiro cha kiti cha urais.

Rais Joyce Banda ametaka kura hizo kuhesabiwa upya bila ya kutumia mitambo ya elektroniki ya kuhesabu kura.
Bi Banda alikumbwa na ushindani mkali katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumanne kutoka kwa wagombea watatu akiwemo, waziri wa zamani wa mambo ya nje Peter Mutharika.