Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hii ni katika hatua ya kuingia katika hatua ya pili ya wananchi wa Yemen kuipinga serikali yao na kuonyesha kuto ridhika kwa wananchi hao dhidi ya Rais wa nchi hiyo (Abd Rabbuh Mansur Al-Had) wananchi hao wamefanya maandamano hayo makubwa yaliofanyika baada ya sala ya Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo Sana`a na baadhi ya mikoa mingine nchini Yemen.
Maandamano hayo makubwa yamifanyika kwakuandaliwa na kikundi cha Ansarul Allah nchini humo wakipinga hatua yeyote ya kupuuzwa mitazamo na matashi yao wakisisitiza kupinga vitendo vya kuchelewesha utekelezaji wa miswada iliopitishwa na wananchi wote.
Hivi karibuni wananchini wa Yemen walifanya maandamano makubwa kupinga matumizi mabaya ya mali za uma na kuto tatuliwa matatizo ya kijamii na kisiasa kupitia serikali ya nchi hiyo pia kutotekeleza makubaliano yaliopitishwa kitaifa.
Abd Rabbuh Mansur Al-Had Rais wajamhuri ya Yemen wiki iliopita aliamuru serikali na waziri mkuu kujiuzuru ama wananchi na jumuiya ya Mahuthiy (mashia wa Yemen) wasema kuwa hatua hiyo ni kupuuza matashi na maamuzi ya wananchi huku wakisisitiza kuwa wataendelea kupinga mpaka kutekelezwa matakwa ya wananchi.
Haya yote ni katika hali ambayo kamati ya maandamano ya wananchi wa Yemen wametangaza kuwa siku ya Jumapili na Jumamosi kutakuwa na mjumuiko mkubwa wa maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo Sana`a nchini humo dhidi ya Rais wa Jamhuri ya nchi hiyo.
5 Septemba 2014 - 22:26
Msimbo wa Habari: 635769
Maandamano makubwa ya mashia wa Yemen yamefanyika baada ya kumaliza sala ya Ijumaa kwaajili ya kupinga siasa na mienendo ya serikali