3 Oktoba 2014 - 12:21
Kiongozi wa Boko Haram: bado niko hai

Kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Boko Haram katika ujumbe wake wa video yake baada ya kusisitiza kuwa yeye bado yuko hai amesema kuwa yeye ndiye kiongozi na amiri wa utawala wa ukhalifa (serikali ya kiislam) ambapo mpaka sasa maeneo kadhaa yako chini yao katika nchi hiyo ya Nigerian.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: katika hali ambayo maafisa wa jeshi la Nigeria wiki iliopita wakitangaza kuuwawa kwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Boko Haram, ama siku ya Alhamisi kiongozi huyo alionekana katika kanda ya video akieleza kuwa yeye bado yuko hai mwenye afya kamili.
Abubakari Shikavo kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Boko Haram amabaye anapambana na jeshi la Nigeria ametuma ujumbe wake kwa utawala wa Nigeria naye katika kanda hiyo baada ya kusistiza kuwa bado yuko hai alisema uongozi wa ukhalifa wa kiislamu uko mikononi mwake, naye amesema kikundi hicho kimefanikiwa kumiliki na kusambaa katika mikoa kadhaa na sehemu nyengine mbali mbali nchini Nigeria.
General Chris msemaji mkuu wa jeshi la Nigeria alitangaza kuwa Boko Haram walikuwa katika juhudi za kukiteka kijiji cha Kandoja kilichopo karibu nan chi ya Cameron , lakini jeshi la anga na ardhi lilipambana na magaidi hao hatimaye kupelekea kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Boko Haram kupoteza maisha katika mapambano hayo.
Abubakari Shikavo amepinga kauli hiyo nakatika kutuma ujumbe wake aliambatanisha na kanda za video zikionyesha akitoa salamu za pongezi kwa viongozi wa vikundi vya kigaidi vya Daesh (Abubakari Albaghda), kikundi cha Al-Qaida (Ayman Al-Zawahiri) na kikundi cha Taliban (Mullah Omar).