Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: shirika la habari la Sky News limetangaza kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh wameonekana wakinyanyua bendera zao nyeusi wakitembea katika barabara za mji wa Darnah mashariki mwa Libya, huku wakitanza uwepo wao katika nchi hiyo.
Magaidi hao wamefanikiwa kumiliki mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli na baadhi ya sehemu ya mkoa wa Benghazi na mpaka sasa bado kunamapegano baina ya magaid hao na majeshi ya Libya.
Tatizo kubwa liliopo hivi sasa nchini Libya ni suala la kuto kuwa na Amani na utulivo nchini humo, kwani imekuwa kila wakati hutokea mapigano na vikundi vya kigaidi vyenye silaha katika makao makuu ya nchi hiyo Tripoli na Benghazi, hali ambayo inatishia mustakabali wa nchi hiyo hasa baada ya tukio hili la daesh kutangaza uwepo wake nchini humo.
6 Oktoba 2014 - 20:13
Msimbo wa Habari: 642652
Magaidi wa Daesh watangaza uwepo wao nchini Libya huku wakionekana na bendera zao wakiwa wamepanda magari wakizunguka katika barabara za mji wa Darnah nchini Libya mji ambao hivi sasa uko chini ya vikundi vilio beba silaha nchini humo