23 Oktoba 2014 - 07:24
Jeshi la Syria latungua ndege mbili za Magaidi

Waziri wa upepelezi wa Syria amesema kuwa: Jeshi la Syria limeziangusha ndege mbili za kivita za magaidi wa Daeshe.

Waziri wa upepelezi wa Syria amesema kuwa: Jeshi la Syria limeziangusha ndege mbili za kivita za magaidi wa Daeshe.
Ndege hizo ambazo ziliibiwa na magaidi hao kutoka katika jeshi la Syria, zimeangushwa katika mji wa Halab wakati magaidi wanafanya mazoezi ya kutumia ndege hizo.
Kikundi cha magaidi cha Daesh ambacho kinapata udhamini kutoka kwa Saudia Arabia, Uturuki na Qatar kilifanikiwa kuiba ndege tatu za jeshi la Syria, ambapo kwa sasa mbili zimekwisha teketezwa.
Imran Zaabiameongeza kusema kuwa halina hofu na ndege iliyobakia kwani si tishio tena.
Ni muhimu kuashiria kwamba magaidi wa Daesh wanawatumia marubani wa zamani wa utawala wa Saddam Husein kuendesha ndege hizo za kivita, Pia Jeshi la Syria limeendelea kusonga mbele katika mapambano yake ya nchi kavu dhidi ya magaidi hao.