12 Novemba 2014 - 16:34
 Mayahudi wachoma msikiti Parestina + Picha

Walowezi wa Kiyahudi wameutia moto msikiti katika Ukingo wa Magharibi kwa kile kinachoonekana kuwa ni shambulio la kulipiza kisasi wakati mzozo kati ya Wapalestina na Israel ukizidi kushtadi.

Walowezi wa Kiyahudi wameutia moto msikiti katika Ukingo wa Magharibi kwa kile kinachoonekana kuwa ni shambulio la kulipiza kisasi wakati mzozo kati ya Wapalestina na Israel ukizidi kushtadi.
Machafuko hayo yaliokuweko kwa miezi kadhaa sasa yamepamba moto katika siku za hivi karibuni kwa kuenea kutoka Jerusalem ya mashariki hadi kwenye Ukingo wa magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel na katika maeneo ya Israel wanakoishi watu wa jamii ya kiarabu na kuzusha hofu ya kuzuka mapigano mazito ambayo yatakuwa ni radiamali na majibu ya waparestina kwa kuchomewa msikiti wao.
Katika hotuba ilionyeshwa na televisheni jana usiku Waziri Mkuu wa Israel Benjami Netanyahu amesema ameamuru kuchukuliwa kwa hatua kadhaa za usalama nchini kote kupambana na maandamano yanayozidi kuongezeka katika eneo hilo.
Shambulio hilo la kuteketeza msikiti lililotokea alfajiri karibu na makazi ya walowezi ya Kiyahudi ya Shilo, Shambulio hilo la kuchoma nyumba tukufu ya ibada za waislamu limekuja baada ya mashambulizi mawili tafauti yaliyotukia siku ya Jumatatu ambapo Wapalestina waliwapiga visu na kuua mlowezi wa kike wa Kiyahudi kusini mwa Ukingo wa magharibi na mwanajeshi wa Israel mjini Tel Aviv.
Afisa wa usalama amesema walowezi waliteketeza kabisa ghorofa ya chini ya msikiti huo katika kitongoji cha Al-Mugheyr karibu na mji wa Ramallah ulioko Ukingo wa magharibi na polisi wa utawala wa Israel wamethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.
Shambulio dhidi ya msikiti linakuja wakati ghadhabu ya Wapalestina ikitokota kutokana na vikosi vya Israel kumuua kwa kumpiga risasi muandamanaji wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 22 kusini mwa Ukingo wa magharibi hapo Jumanne.
Yafaa kuashiria kuwa: Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameelekea nchi jirani ya Jordan kwa mazungumzo na Mfalme Abdulla ambayo yanatarajiwa kulenga hali ya machafuko hayo inayozidi kupamba moto kati ya utawala wenye maguvu wa Israel na raia wasio jiweza wa Parestina pamoja na mashambulizi yanayoongozwa na Marekani dhidi ya magaidi wa Daesh wanaofanya mashambulizi yao nchini Iraq na Syria.
Jordan ambayo dhima yake ni mlezi wa maeneo matakatifu ya Waislamu yaliyoko Jerusalem ya mashariki kama ilivyotajwa katika mkataba wa amani wa mwaka 1994 na Israel, imeelezea wasi wasi wake juu ya hatua ilizochukuwa Israel katika eneo takatifu la msikiti wa Al Aqsa lililozusha mapambano.
Kampeni ya makundi ya Kiyahudi ya sera kali za mrengo wa kulia ya kutaka kupatiwa haki ya kufanya ibada ndani ya eneo hilo ambalo ni mojawapo ya maeneo nyeti kabisa Mashariki ya Kati imechochea mvutano ambao tayari ulikuwa mkubwa kwa sababu ya kutanuliwa kwa makaazi ya walowezi ya Kiyahudi katika eneo la Jerusalem ya mashariki lililotwaliwa na Israel, pamoja na kuwepo kauli za kuikataza serikali ya Israel isiendelee kujenga makazi katika maeneo ya taifa la waparestina, serikali ya Israel imeziba masikio na kuendelea kuvunja nyumba za raia wasiojiweza wa kiparestina na kujenga nyumba na makazi mapya ya Mayahudi, hii ni kinyume na haki za binadamu pia ni kinyume na kanuni za umoja wa mataifa.