Shireika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Ahmad Daudi Ughlu waziri mkuu wa Uturuki siku ya Jumapili baada ya kuonana na Obama na kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa vyombo vya habari amesema: sisi katika suala la kuondoka madarakani Rais wa Syria na magaidi wa Daesh nchini Syria hatutafautiani na serikali ya marekani katika suala hilo, pia Obama alisha zungumzia udharura wa kutolewa madarakani kwa Rais huyo wa Syria.
Kabla ya Siku moja kupita mazungumzo ya waziri mkuu wa Uturuki Obama amepinga mazungumzo hayo katika maelezo yake alioyatoa siku ya Jumanne akibainisha kuwa sisi katika swala zima linalo husu utawala wa Syria mpaka sasa hatuna mabadiliko yoyote, na hatujakuwa na muafaka wa kumtoa madarakani Rais Assad wa Syria, kwani hivi sasa tunafikiria njia muhimu ya kuwasambaratisha magaidi wa Daesh nchini Syria na Iraq.
Kukanusha kwa Rais wa Marekani Baraka Obama madai ya waziri mkuu huyo wa Uturuki kumepelekea kukosolewa vikali katika mitazamo ya watu wote pia vyombo vya habari pote ulimwenguni.
19 Novemba 2014 - 21:02
Msimbo wa Habari: 652501
Rais Baraka Obama wa Marekani amebainisha na kukanusha maelezo ya waziri mkuu wa Uturuki kuwa marekani na Uturuki yaafikiana kupanga mbinu za kumtoa madarakani Rais wa Syria Bashar Al-Assad