25 Novemba 2014 - 19:40
Umoja wa Ulaya waendelea na vikwazo dhidi ya Iran

Umoja wa Ulaya umerefusha hatua ya kuzuwia baadhi ya mali za Jamhuri ya kiislamu Iran ikiwa ni sehemu ya vikwazo dhidi ya nchi hiyo, baada ya mazungumzo yenye lengo la kupunguza harakati za mpango wa nyuklia wa nchi hiyo kurefushwa kwa miezi saba.

  Umoja wa Ulaya  umerefusha  hatua ya kuzuwia baadhi ya mali za Jamhuri ya kiislamu Iran ikiwa ni sehemu ya vikwazo dhidi ya nchi hiyo, baada ya mazungumzo yenye lengo la kupunguza harakati za mpango wa nyuklia wa nchi hiyo kurefushwa kwa miezi saba.

Kurefushwa kwa vikwazo hivyoni pamoja na kupigwa marufuku biashara ya mafuta, dhahabu na  baadhi ya shughuli za fedha.

  Mataifa 28 ya Umoja wa ulaya yamerefusha vikwazo  hivyo hadi Juni 30 mwaka ujao 2015. Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani zilishindwa kufikia makubaliano ya nyuklia jana mjini Vienna , ambayo yangemaliza mvutano wa miaka 12  na sasa pande hizo zimejiongezea muda  kuyapa nafasi makubaliano hayo.

Mataifa hayo sita yanayozungumza na Iran ni Marekani, Ufaransa, Uingereza, Urusi, China  na Ujerumani.

  Mataifa ya Ulaya na Malekani yamezuia mali za Iran zilizokatika mabenki ya nje na kuwawekea vikwazo vya kutouza bidhaa na kutonunua bidhaa ikiwa kama adhabu ya kuifanya serikali hii iachekutengeneza makombora ya nyuklia ambayo inahofiwa kuwa ni hatari hasa kwa adui namba moja wan chi hiyo ambaye ni Israel na Marekani.

  Jamhuri ya kiislamu ya Iran imekuwa ikipinga shutuma za kutaka kutengeneza makombora ya nyuklia, hata hivyo kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya Iran ayatollah Khamenei hakuwa na matumaini kabisa na mazungumzo ya nyuklia na aliwataka wananchi wake kujitahidi kujenga ujumi wao wa ndani na kuacha kutegemea mali zao zilizozuiliwa na maadui wa maendeleo ya taifa hilo la kiislamu lenye nguvu.

 

Tags