Wabunge wa Somalia wamepiga kura ya kumtoa madarakani waziri mkuu wa nchi hiyo kwa mara ya pili ndani ya mwaka mmoja, katika hatua ambayo wafadhili wa magharibi wameonya inaweza kuvuruga zaidi utengamano dhaifu wa taifa hilo lililoharibiwa na vita.
Waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed amekuwa katika mzozo na rais Hassan Sheikh Mohamud, kuhusiana na mabadiliko katika baraza la mawaziri, mabadaliko ambayo rais aliyatangua.
Waziri mkuu huyo amekuwa madarakani kwa muda wa chini ya mwaka moja tu, baada ya kufukuzwa mtangulizi wake, ambaye pia alizusha mabishano juu ya muundo wa baraza la mawaziri, na kutuhumiwa kwa utendaji mbaya.
Spika wa bunge la Somalia Mohamed Sheikh Osman Jawari, amesema waziri mkuu na baraza lake wamefukuzwa baada ya wabunge 153 kuupigia mswada huo, dhidi ya 80 waliomuunga mkono, na kumtaka rais aunde serikali mpya haraka iwezekanavyo.