Watu saba wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya mripuaji wa kujitoa mhanga jana kujiripua katika msikiti mmoja wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia mjini Rawapalpindi nchini Pakistan.
Mripuko mkubwa ulisababisha mtafaruku wakati kundi la watu kadhaa wa jamii ya wachache ya Washia waliokuwa wamekusanyika katika msikiti huo wakitoa sadaka kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtume Mohammad s.a.w. Afisa tawala mwandamizi katika mji huo Sajid Zafar Dall aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba kulikadiriwa kuwa na kati ya watu 100 hadi 150 wakati kadhia hiyo ikitokea msikitini humo. Maafisa wengine wanasema miongoni mwa waliojeruhiwa wamo polisi waliokuwa wakiulinda msikiti huo na kwamba majeruhi wamesamabazwa kwa ajili ya matibabu katika vituo mbalimbali. Pakistani imezidisha mashambulizi yake dhidi ya wanamgambo wa Taliban, tangu wafanye shambulio la Desemba 16 lililosababisha vifo vya watu 150 wakiwemo watoto 134.
Imekuwa ni kama ada ya wafuasi wa dhehbu la Sunni hasa wale wenye siasa kali kuwaua waislamu wenzao wa dhehebu la Shia, hii inatokana na fikra potovu zinazotangazwa na mashekhe na viongozi wa dini wa dhehebu la Sunni kwa waumini wao kuwa Mashia ni makafiri na ni thawabu kuwaua, wafuasi wa dhehebu la Sunni huchua maneno ya mashehe wao bila kuchuja na kujikuta wanaua waislamu wenzao na kusahau kwamba uislamu halisi wa mtume Muhammad s.a.w si tukwamba unapinga kumuua muislamu mwingine bali unapinga kumuua hata asiyekuwa muislamu.