31 Januari 2015 - 10:56
Zaidi ya watu 20 wauwawa Ukraine

Zaidi ya watu 20 wanaripotiwa kuuwawa katika mapigano mapya yaliyozuka jana huko mashariki mwa Ukraine, na kuzusha mashaka ya uwepo wa duru mpya ya mazungumzo ya amani baina ya pande zinazohasimiana nchini humo.

Viongozi wa wanamgambo katika ngome yao ya Donestsk wamesema kiasi ya raia saba wameuwawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa na makombora yaliorushwa karibu na kiberenge cha abiria na kituo cha misaada. Kama ilivyokuwa katika matukio yaliyopita pande zote mbili zinatuhumiana kufanya shambulizi hilo.

Kwa upande wa wanaotaka kujitenga wa Donetsk wanasema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuvizingira vikosi vya jeshi la serikali katika eneo la kimkakati la Debaltseve, eneo la reli lenye kuunganisha upande huo na wilaya nyingine zinazodhibitiwa na serikali kwa barabara moja tu.