26 Februari 2015 - 19:16
Katibu mkuu wa NATO aionya Urusi

Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amneonya kwamba jaribio lolote la kupanua mipaka inayoshikiliwa na wapiganaji wanaotaka kujitenga nchini Ukraine ,

Katibu  mkuu  wa  NATO Jens Stoltenberg  amneonya  kwamba jaribio  lolote  la  kupanua  mipaka  inayoshikiliwa  na  wapiganaji wanaotaka  kujitenga  nchini  Ukraine , hazitakubalika  na kuiambia Urusi  kuondoa  vifaa  1,000  vya  kijeshi  kutoka  katika  ardhi  ya nchi  jirani  ya  Ukraine.

Akizungumza  baada  ya  mkutano  na  waziri  mkuu  wa  Italia Matteo Renzi , katibu  mkuu  wa  NATO  ameeleza  matumaini ya tahadhari  juu  ya  matarajio  ya  makubaliano tete  ya  kusitisha mapigano  kati  ya  waasi  wanaoungwa  mkono  na  Urusi  na majeshi  ya  Ukraine.

O-Ton Stoltenberg

Matamshi  ya  Stoltenburg  yanakuja  wakati  jeshi  la  Ukraine limetangaza  kuanza  kuondoa  silaha  kali  kutoka  katika  mstari  wa mbele  wa  mapambano.

Nahuko Ugiriki mpango  wa  utatuzi wa matatizo ya uchumi wa Ugiriki  unaotarajiwa  kurefushwa  kwa  miezi  minne unatazamiwa  kupata  uungwaji  mkubwa  mkono katika  bunge  la Ujerumani  baada  ya  idadi  kubwa  ya  wabunge  katika  chama  cha kihafidhina  cha  kansela  wa  Ujerumani Angela Merkel  kuonesha ishara  ya  kuunga mkono.

Bunge litapiga  kura  Ijumaa  katika  makubaliano  yaliyofikiwa  na mawaziri  wa  fedha  wa  mataifa  wanachama  wa  sarafu  ya  euro. Volker Kauder, kiongozi  wa  wabunge  wa  chama  cha  kansela Merkel , amesema  wengi  wa  wabunge  wa  chama  hicho wataunga  mkono  makubaliano  hayo. 

Muungano wa  vyama  vinavyounda  serikali  inayoongozwa  na chama  cha  kansela  Merkel  ikiwa  ni pamoja  na  chama cha  siasa za  wastani  za  mrengo  wa  shoto  cha  Social Democratic  SPD, chama  ambacho kinaunga mkono  kwa  dhati  mapendekezo  hayo, una jumla  ya  robo  tatu  ya  viti  bungeni.

Wakati  huo  huo Wabunge  nchini  Uholanzi  wamepiga  kura  leo kuunga  mkono  urefushaji  kwa  miezi  minne mpango  wa  uokozi wa  uchumi  wa  Ugiriki.