Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Kwamujibu wa tovuti ya kimarekani ya Hill News msaidizi huyo alisema siku ya ijumaa mjini washinton Mrekani kwamba: kama makubaliano yatafikiwa katika suala la nyukilia ya Iran, dunia itahukumu kuwa jambo hili ni jema na nimaslahi ya dunia. Na hiyo ndio njia pekee itakayo tuthibitishia kuwa Iran aina niya ya kutengeza silaha za nyukilia na haitatengeza silaha hizo, kwani hakuna njia nyingine ya kututhibitishia suala isipokuwa njia hiyo.
Tovuti hiyo imeandika kuwa maelezo ya Wendy Sherman yamejiri baada ya juhudi kubwa ya kikundi cha 5+1 katika kufikia makubaliano baina yao na Iran katika masuala ya nyukilia.
1 Machi 2015 - 19:45
Msimbo wa Habari: 674152
Msaidizi wa masuala ya kisiasa wa wazirir wamambo ya nje ya Marekani (Wendy Sherman ) ambaye ni mmoja kati ya wajumbe wa timu ya mazungumzo ya nyukilia ya Iran na kundi la 5+1 aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano kuhusu masuala ya nyukilia ya Iran ametangaza kuwa: kama muafaka utafikiwa naamini kuwa dunia itapongeza muafaka wa kidiplomasia baina ya Irana na kikundi cha 5+1