2 Machi 2015 - 19:00
Jenerali Haftar ateuliwa kama kamanda mkuu wa jeshi Libya

Jenerali wa zamani nchini Libya Khalifa Haftar amethibitishwa leo kuwa kamanda mkuu wa jeshi la serikali ya nchi hiyo inayotambuliwa kimataifa.

Jenerali  wa  zamani  nchini  Libya  Khalifa Haftar  amethibitishwa leo kuwa  kamanda  mkuu  wa  jeshi  la  serikali  ya nchi  hiyo inayotambuliwa  kimataifa.

Hatua  hiyo  ya uteuzi  wa  Haftar , mshirika  wa  zamani  wa kiongozi  wa  Libya  Muammar Gaddafi  ambaye  baadaye  alijiunga na  vuguvugu  la  mapinduzi  dhidi  ya   kiongozi  huyo  wa  Libya, unaweza  kuweka  ugumu  katika  juhudi  za  Umoja  wa  Mataifa kufikia  makubaliano  kati  ya  serikali  mbili   hasimu  za  nchi  hiyo.

 Haftar  ameunganisha  jeshi  lake  la  kawaida  na  vikosi  vya  jeshi la  serikali  upande  wa  mashariki kupambana  na  makundi  ya itikadi  kali  ya  Kiislamu. Pia  amelilenga  kundi  la  Libya  alfajiri, ambalo  limeukamata  mji  mkuu  Tripoli na  kuunda  serikali hasimu.