9 Machi 2015 - 21:19
Marekani ndio chanzo cha matatizo mashariki yakati

Rais wa harakati za kisiasa dhidi ya utanda wazi nchini Urusi amesema: Marekani ndio chanzo cha ugaidi na kuleta matatizo katika ukanda wa mashariki ya kati

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kiongozi Alexander ameyasema hayo katika kipindi cha kisiasa katika televishen ya taifa nchini Urusi nakusisitiza kuwa: Marekani katika kipindi hiki amesababisha vita na matatizo sehemu nyingi duniani matatizo ambayo yamesababisha kupoteza maisha ya mamilioni ya watu na kuleta uharibifu mkubwa katika maeneo hayo.
  Aidha amebainisha kuwa Marekani hutumia njia mbalimbali kwaajili ya kulinda maslahi yake ikiwemo kuanzisha vita ya wenyewe kwa wenyewe katika baadhi ya maeneo.
Naye alisema Marekani ndio mwanzilishi wa vikundi vya kigaidi vya Daesh katika mashariki ya kati, kwani wamewekwa na serikali ya Marekani katika kufikia malengo yao ya kisiasa, serikali ya Marekani imefanya uvamizi mwaka 2011 nchini Libya na baada ya kuanguka utawala wa Libya Marekani ikatengeza vikundi vitano vya kigaidi nchini humu kwaajili ya kuhifadhi maslahi yao.
Kiongozi huyo wa harakati ya kisiasa dhidi ya utandawazi akibainisha kuwa Marekani inatumia kila njia kuizui Urusi kushika nafasi ya awali katika nyanja za kimataifa alisema: Urusi mpaka sasa imeshika nafasi yake kisiasa katika nyanja za kimatifa kama ilivyokuwa hapo zamani.