Mataifa ya Magharibi yamependekeza programu ya msaada wenye thamani ya euro bilioni 38 kwa Ukraine, bilioni 15 na nusu zikitoka Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF. Mkuu wa shirika hilo, Christine Lagarde, alitangaza hapo jana jijini Berlin, kwamba Bodi ya Wakurugenzi ya IMF imekubaliano juu ya mpango huo. Kwa mujibu wa Lagarde, Ukraine imefanikiwa kutunza nidhamu ya kifedha licha ya hali ngumu iliyonayo. Programu hii inachukuwa nafasi ya mpango wa awali wa euro bilioni 15 na nusu ulioongezewa muda mwaka jana, kuisaidia Ukraine kudhibiti uchumi wake ulioathiriwa na mageuzi ya kisiasa na mzozo wake na waasi wa mashariki wanaotaka kujitenga.
12 Machi 2015 - 14:37
Msimbo wa Habari: 676368
Mataifa ya Magharibi yamependekeza programu ya msaada wenye thamani ya euro bilioni 38 kwa Ukraine