12 Machi 2015 - 21:12
Daesh wanatoakana na tamaduni za Ulaya

Mwandishi mmoja wa gazeti ambaye alikuwa ametekwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh na baadae kuachwa huru amesema alipokuwa akiojiwa kuwa kikundi cha Daesh ni kimezalika kutoka katika tamaduni za Ulaya

Shirika la habari AhluBayt (a.s) ABNA: hayo ameyasema (Nicholas) mwandishi wa magazeti nchini Ufaransa ambae alitekwa nakuwa chini ya Daesh kwa miezi 10 alipokuwa akifanya maojiano na vyombo vya habari
Aidha aliendelea kubainisha kuwa kipindi alichokuwa alifahamu kuwa Daaesh hawana uhusiano na tamaduni ya kiislamu wala yakiarabu kwakusema: nilipokuwa nikizungumza nao nilikuja fahamu kuwa wao hawana alama yoyote inayohusika na tamaduni za kiislamu na uarabu , bali wao ni watu kutoka katika jamii yetu, kwani wana kila alama za jamii yetu hata huzungumza lugha yetu kiasi kwamba hata zile lahaja wasioweza kuzitamka watu waliojifunza lugha zetu wao walikuwa wakizitumia, pia wao huangalia filamu zilezile sisi tunaangalia, hucheza magemu yaleyale tunayocheza sisi nami bilashaka nawaambia kuwa wao ni watoto wa tamaduni zetu za Ulaya.