13 Machi 2015 - 18:50
Magaidi wa Daesh waahidi kuzishambulia nchi za Magharibi

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wameahidi kuendelea kufanya mashambulio katika nchi za magharibi.Msemaji wa magaidi hao wa itikadi kali amesema katika risala yao mpya

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wameahidi kuendelea kufanya mashambulio katika nchi za magharibi.Msemaji wa magaidi hao wa itikadi kali amesema katika risala yao mpya,wanapanga kuishambulia Ikulu ya Marekani mjini Washington na mnara mashuhuri wa saa wa mjini London-Big Ban, miongoni mwa shabaha nyingine.Wakati huo huo magaidi hao wa kundi la kigaidi la Daesh wamelikubali pendekezo la utiifu la Boko Haram.Kiongozi wa kundi la kigaidi la Daesh,Abu Bakr al Baghdadi " amesema amekubali "kiapo cha utiifu" cha ndugu zao wa Nigeria.Katika risala iliyochapishwa mwishoni mwa wiki iliyopita Boko Haram wamewahakikishia kundi la kigaidi la Daesh unyenyekevu wao kwao na kujiunga pamoja nao.