Viongozi wa taifa na serikali wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekubaliana kurefusha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi hadi Desemba mwaka huu.Katika mkutano wao wa kilele mjini Brussels viongozi hao wa mataifa 28 wamefungamanisha vikwazo hivyo na kuheshimiwa makubaliano ya Minsk ya kuweka chini silaha na kurejesha amani Mashariki ya Ukraine.Kwa namna hiyo viongozi wa Umoja wa Ulaya wanataka kuzidi kumshinikiza rais Vladimir Putin wa Urusi atumie ushawishi wake kuwatanabahisha waasi wanaoelemea upande wa Urusi ili kumaliza mzozo wa Mashariki ya Ukraine.Uamuzi wa viongozi wa taifa na serikali unabidi kwanza upate ridhaa ya baraza la mawaziri wa Umoja wa Ulaya.Muda wa vikwazo hivyo ulipangwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa julai ujao.Inakadiriwa vikwazo hivyo vimeilisha Urusi hasara ya mabilioni kadhaa hadi sasa.
20 Machi 2015 - 11:25
Msimbo wa Habari: 677977
Viongozi wa taifa na serikali wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekubaliana kurefusha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi hadi Desemba mwaka huu.