Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya Bernardino Leon ameonya hii leo kuwa pande mbili zinazozana nchini Libya ziko mbali kufikia makubaliano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa huku duru nyingine ya mazungumzo ya kuzikutanisha pande hizo ikianza jana nchini Morocco. Leon amesema kufikiwa kwa makubaliano itakuwa kibarua kigumu na bado safari ni ndefu ya kukubaliana namna ya kuunda serikali ya muungano wa kitaifa. Huku mazungumzo hayo ya siku tatu yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa yakiendelea Morocco, serikali ya Libya inayotambulika na jumuiya ya kimataifa imesema imeanzisha mashambulizi ya kijeshi ya anga ya kuukomboa mji mkuu Tripoli uliotekwa na waasi mwaka jana.
21 Machi 2015 - 19:51
Msimbo wa Habari: 678262
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya Bernardino Leon ameonya hii leo kuwa pande mbili zinazozana nchini Libya ziko mbali kufikia makubaliano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa huku duru nyingine ya mazungumzo ya kuzikutanisha pande hizo ikianza jana nchini Morocco.