Rais Barack Obama wa Marekani amemkosoa wazi wazi waziri mkuu aliyechaguliwa tena wa Israel Benjamin Netanyahu,alipokuwa anazungumzia uungaji mkono wa nchi yake kwa ufumbuzi wa "madola mawili" kwa mzozo wa mashariki ya kati.Katika mahojiano na gazeti moja la Marekani rais Obama amesema, tamko la Netanyahu dhidi ya kuundwa dola ya Palestina, alilolitoa mwishoni mwa kampeni ya uchaguzi,limeyazika matumaini ya utaratibu wa amani pamoja na wapalestina.Amemkumbusha hayo Netanyahu baada ya ushindi wake, kwa kusema,kwamba ufumbuzi wa madola mawili ndio njia pekee itakayoihakikishia Israel usalama wake.Ingawa Marekani inataka kuendelea kushirikiana na Israel,hata hivyo lakini inaendelea kuamini hali iliyo haivumiliki hata kwa kuzingatia kikamilifu usalama wa Israel. Rais Obama ameonya hali hiyo haisaidii kuleta utulivu katika eneo hilo.
Israel imechukua ardhi ya Palestina kwa nguvu na sasa inapinga kabisa taifa la Palestina kutambulika, kwani inataka kuchukua ardhi yote ya Palestina na kusiwe kabisa na jina la Palestina.