25 Machi 2015 - 11:28
Magaidi wa Daesh wadai kuhusika na mashambulizi Libya

Wanamgambo wanaolitii kundi la kigaidi lenye itikadi kali la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu

Wanamgambo wanaolitii kundi la kigaidi lenye itikadi kali la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu, wamedai kuhusika na shambulizi la kujitoa muhanga lililotokea jana katika mji wa mashariki mwa Libya, Benghazi na kuwaua watu saba. Taarifa ya kundi hilo iliyotolewa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter, imeonyesha picha za shambulizi hilo pamoja na mshambuliaji aliyejitoa muhanga. Shambulizi hilo limesababisha vikosi vya jeshi la Libya kujibu kwa mashambulizi ya anga. Shambulizi hilo limetokea saa chache baada ya Umoja wa Mataifa kuwasilisha mpango wa mapendekezo sita yenye lengo la kumaliza ghasia nchini Libya, kwa kuanzisha serikali ya mpito itakayotawala hadi katiba mpya itakapopatikana na uchaguzi utakapofanyika.