28 Machi 2015 - 18:40
 Mazunguzo ya nyuklia ya Iran yaendelea Uswis

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier leo hii amejumuika katika mazungumzo ya nyuklia na Iran nchini Uswisi ambapo amesema mazungumzo hayo yapo katika hatua ya mwisho.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier leo hii amejumuika katika mazungumzo ya nyuklia na Iran nchini Uswisi ambapo amesema mazungumzo hayo yapo katika hatua ya mwisho. Steinmeier aliwaambia hayo waandishi wa habari kabla ya kujiunga na mawaziri wenzake wa Marekani, Ufaransa na Iran mjini Lausanne ikiwa zimebakia siku chache kabla ya siku ya mwisho ya kufikia maazimio ya makubaliano hayo Jumanne ijayo. Aidha aliongeza kusema kuhitimishwa kwa mafanikio kwa mazungumzo ya nyuklia ya Iran yaliyodumu kwa muda mrefu kunaweza kuleta utulivu kwa kiasi fulani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Iran ni moja kati ya nchi zenye nguvu ya kijeshi na ushawishi wa hali ya juu wa kisiasa katika mashariki ya kati, hivyo kufikia makubaliano na Iran, kutapelekea kupatikana suluhisho la amani mashariki ya kati, hii inatokana na mataifa mengi ya kiarabu hasa yanayidhulumiwa kuwa karibu na Iran kutokana na utetezi wake kwa mataifa hayo.