Israel imekosoa vikali makubaliano yaliyofikiwa kuhusu mradi wa nyuklia wa Iran.Usalama wa Israel umeingia hatarini kutokana na makubaliano hayo, amesema waziri mkuu wa Israel katika mazungumzo ya simu pamoja na rais Barack Obama wa Marekani .Makubaliano hayo yanahalalisha mradi wa nyuklia wa Iran na yatapelekea kutokea uchokozi mkubwa zaidi Mashariki ya kati,anasemaBenjamin Netanyahu na kuongeza tunanukuu"yanaweza hata kusababisha vita ". Mwisho wa kumnukuu waziri mkuu wa Israel.
Rais Obama ameutaja mwongozo wa makubaliano pamoja na Iran kuwa ni "hatua ya kihistoria."
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani pia amesema "walimwengu hivi sasa wanakurubia kufikia makubaliano halisi kuhusu mradi wa nyuklia,kuliko wakati wowote ule mwengine.
Saudia arabia pia ambayo ni mshirika wa mkubwa wa Marekani na Israel imeyasifu makubaliano hayo pamoja na kwamba nchi ilikuwa ikipinga makubaliano hayo.
Mwongozo huo wa makubaliano pamoja na Jamhuri ya kiislamu ya Iran unaitaka Teheran ipunguze mradi wake wa kinuklea na ikubali kukaguliwa ili badala yake vikwazo vya Marekani, nchi za Ulaya na vile vya umoja wamataifa viondoshwe dhidi ya nchi hiyo ya kiislamu yenye maendeleo ya hali ya juu ya kielimu na teknolojia.
Makubaliano kamili yamepangwa kufikiwa hadi ifikapo mwisho wa mwezi juni mwaka huu.