Mabomu mawili yameripuka katika mji mkuu wa Misri hivi leo siku moja baada ya wanajeshi 15 na raia wawili kuuawa kwenye mashambulizi yaliyotokea katika mji wa Sinai. Miripuko hiyo ya leo mbele ya kituo cha polisi cha wilaya ya Imbaba inaripotiwa kutosababisha maafa yoyote hadi sasa. Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kwa eneo hilo kushambuliwa ambapo mripuko wa mwezi Februari kwenye mgahawa ulipoteza maisha ya mtu mmoja.
Serikali ya Misri inalituhumu kundi la Ikhwanul muslimin kuhusika na mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu dhidi ya maafisa wa usalama, ingawa kundi hilo lililopigwa marufuku linakanusha tuhuma hizo.