5 Aprili 2015 - 20:49
 Wanajeshi wanne wauawa mashariki mwa Ukraine

Wanajeshi sita wa Ukraine wameuawa leo katika matukio mawili tofauti katika eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo wakati machafuko yakiendelea kuvuruga makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu mwaka mmoja sasa.

Wanajeshi sita wa Ukraine wameuawa leo katika matukio mawili tofauti katika eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo wakati machafuko yakiendelea kuvuruga makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu mwaka mmoja sasa. Msemaji wa jeshi la Ukraine amesema wanajeshi wanne waliuawa baada ya gari lao kupigwa na kombora wakati likivuka daraja karibu na eneo linalokaliwa na waasi la Luhansk. Wengine wawili waliuawa baada ya bomu la kutegwa ardhini kulipuka kilomita chache nje ya mji unaodhibitiwa na serikali wa kusini mashariki, Mariupol. Baada ya kuwepo utulivu kwa siku kadhaa katika mgogoro huo mbaya wa Ukraone, vifo hivyo vya karibuni vimefanya  idadi ya wanajeshi waliouawa katika kipindi cha saa 48 kufikia wanane.