Waendesha mashtaka nchini Misri wamefungua mashtaka ya mauaji dhidi ya watu 379 leo kuhusiana na vifo vya polisi na raia wakati wa kuondolewa kwa nguvu waandamanaji katika kambi ya maandamano mjini Cairo mwaka 2013.
Haijafahamika mara moja ni washitakiwa wangapi bado wanashikiliwa na polisi lakini ni wimbi la hivi karibuni kabisa katika mlolongo wa kesi za halaiki kuhusiana na ghasia hizo zilizofuatia jeshi kuupindua utawala wa rais Mohammed Mursi Julai mwaka 2013.
Waendesha mashtaka wanasema washitakiwa walishiriki katika mgomo wa kulikalia eneo wakiwa na silaha katika uwanja wa Nahda mjini humo Agosti mwaka 2013 na kuwashambulia raia katika maandamano katika sehemu mbali mbali mjini Cairo.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeieleza hali hiyo kuwa ni moja kati ya mauaji makubwa ya waandamanaji katika siku moja katika historia ya hivi karibuni.