Umoja wa Mataifa umetaka kusitishwa mara moja kwa mapigano nchini Yemen ili kuruhusu kufikishwa msaada wa dharura kwa maelfu ya watu wenye uhitaji. Shirika la Msalaba Mwekundu na lile la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, lilipatiwa fursa ya kuingia kwenye taifa hilo lililogawanyika katika Bara Arabu. Ndege mbili zilizojaa msaada wa madawa zilitua hapo jana kwenye uwanja wa ndege wa Sanaa, unaoshikiliwa na wanaharakati wa kishia wa Huthi.
Ilikuwa ni shehena ya kwanza ya msaada kwenye mji huo, tangu Saudi Arabia kuongoza muungano wa mataifa ya Kiarabu kuwashambulia raia wa Yemen na wanaharakati wa kishia ili wamkubali rais Hadi tangu mwezi Machi mwaka huu wa 2015. Mapigano kwenye mji wa kusini wa Aden katika wiki za hivi karibuni, yalimlazimisha Rais Abd Rabbo Mansour Hadi ambaye hatakiwi na wananchi wa Yemen, kukimbilia mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh ambapo alikaa kikao na Saudia arabia na Marekani na kuamua kuivamia Yemen kijeshi mpaka imkubali na kumrudisha madarakani.