14 Machi 2016 - 17:01
Watu 37 wauawa kufuatia Mripuko wa bomu Uturuki + Picha

Kiasi yawatu 37 wameuawa na wengine 122 kujeruhiwa baada ya kutokea mripuko wa bomu karibu na kituo cha basi katika mji mkuu wa Uturuki wa Ankara hapo jana usiku

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kiasi yawatu 37 wameuawa na wengine 122 kujeruhiwa  baada ya kutokea  mripuko wa bomu karibu na kituo cha basi katika mji  mkuu wa Uturuki wa Ankara hapo jana usiku. Serikali nchini Uturuki imesema kuwa idadi ya vifo kutokana na  shambulizi hilo la bomu inaweza kuongezeka.  Wengi wa watu waliojeruhiwa katika tukio hilo wanahofiwa kuwa raia ambapo watu wawili wanaoshukiwa kuhusika na mripuko huo nao pia wameuawa katika shambulizi hilo. Hakuna kikundi chochote hadi sasa kilichodai kuhusika na shambulizi hilo ingawa maafisa wa usalama wamewaambia waandishi wa habari kuwa chama cha wafanyakazi cha PKK kilichopigwa marufuku nchini humo kinaweza kuwa kinahusika na shambulizi hilo. Kundi la kigaidi la Daesh ambalo ni swahiba wa serikali ya Uturuki  nalo pia linahusishwa na shambulizi hilo.

Mwisho wa habari/ 291