Shirika la Habari AhlulBayt (a.s) ABNA: taarifa ya kuangamia kwa amiri huyo wa kikundi cha kigaidi imetangazwa leo hii nchini Syria
“Ali Musa Al-sshawakh” amiri wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika wilaya ya Raqqah ameangamia akiwa pamoja na magaidi wengine wa kikundi hicho kutokana na mashambulizi yaliofanywa katika wilaya hiyo.
Siku kadhaa ziliopita (Hasaan Abudiy) amiri wa Daesh katika mji wa Badiya nchini humo pia ameangamia kutkana mashambulio yaliofanywa katika wilaya ya Khanasir ilioko katika mkoa wa Halab nchini Syria.
Wilaya ya Raqqah ni makao makoo ya kikundi cha kigaid cha Daesh nchini Syria, ambapo kuna maelfu ya magaidi wa Daesh kutoka mataifa mbalimbali duniani, ambapo wilaya hiyo imemilikiwa na magaidi hao takriban ni miaka miwili sasa.
mwisho wa Habari/290
22 Machi 2016 - 19:08
Msimbo wa Habari: 742649
Kiogozi wa kikundi cha kigaidi cha Daish katika wilaya ya Raqqah nchini Syria aangamia