23 Oktoba 2016 - 20:51
Mripuko waua afisa wa polisi mashariki mwa uturuki

Maafisa wawili wa polisi wameuawa hii leo huku wengine 10 wakijeruhiwa wakati bomu lililokuwa katika gari liliporipuka jirani na gari la polisi lililokuwa likipita katika jimbo la Bingol mashariki mwa Uturuki.

Shirika la habari la ABNA linaripoti  kuwa: Maafisa wawili wa polisi wameuawa hii leo huku wengine 10 wakijeruhiwa wakati bomu lililokuwa katika gari liliporipuka jirani na gari la polisi lililokuwa likipita katika jimbo la Bingol mashariki mwa Uturuki. Kwa mujibu wa vyombo vya usalama nchini humo bomu lililokuwa limetegwa na wanamgambo wa chama cha wafanyakazi cha Wakurdi kilichopigwa marufuku cha PKK liliripuka jirani na ofisi ya Gavana katika mji huo. Polisi sita ni miongoni mwa waliojeruhiwa katika tukio hilo. Mji huo wa kusini mashariki mwa Uturuki unaokaliwa zaidi na wakurdi umekuwa katika hali ya vurugu tangu kusambaratika kwa mazungumzo ya amani yenye lengo la kusitisha mapigano kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa PKK mwaka jana. Uturuki, Marekani na Ulaya wanawachukulia wanamgambo wa chama cha PKK kama magaidi. Zaidi ya watu 40,000 wengi wao wakurdi wameuawa nchini humo tangu wanamgambo hao walipoanzisha mashambulizi dhidi ya serikali miongo mitatu iliyopita.

Mwisho wa habari/ 291