2 Novemba 2016 - 20:14
Trump aongoza kwa katika kura ya maodni dhidi ya Clinton

Kampeni za Uchaguzi wa Marekani zimejaa kejeli, maneno machafu na kashfa jambo linaloashiria kuporomoka kwa maadili ya nchi hiyo kubwa duniani.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kwa mujibu wa utafiti mpya wa maoni mgombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican Donald Trump anaongoza kwa asilimia ndogo katika kinyang'anyiro cha urais. Utafiti wa gazeti la Washington Post na kituo cha televisheni cha ABC, umeonyesha Trump amempita mpinzani wake Hillary Clinton kwa pointi 1, Hata hivyo utafiti mwingi unaonyesha kuporomoka kwa ushindi wa jimbo kwa jimbo mgombea wa Democratic Bi Clinton ambao unadhihirisha umuhimu katika mfumo wa uchaguzi wa taifa hilo. Kunyanyuka kwa Trump kumekuja baada ya shirika la upelelezi la nchini humo FBI kutoa taarifa kuwa wamegundua barua pepe mpya binafsi za Bi Clinton ambazo wanazifanyia uchunguzi mpya. Barua hizo pepe zilikutwa katika kompyuta ya Antony Weiner aliyekuwa mume wa msaidizi wa bi Clinton Huma Abedin. Zimesalia siku sita kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa urais hapo Novemba nane.

Kampeni za Uchaguzi wa Marekani zimejaa kejeli, maneno machafu na kashfa jambo linaloashiria kuporomoka kwa maadili ya nchi hiyo kubwa duniani.

Mwisho wa habari/ 291