Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Magaidi wanaoungwa mkono na Marekani nchini Syria wamekabiliana vikali na vikosi vya serikali katika mji wa Aleppo, ambapo mashambulizi yaliyofanywa na vikosi vya serikali yamesababisha vifo vya magaidi hao zaidi ya 150, na kuacha miili yao ikitapakaa kwenye viunga vya mji huo, huku Marekani ikiendelea kutafuta njia za kuwanusuru magaidi hao na hujuma kali za serikali.
Mashambulizi yanayofanywa na serikali kwenye mji uliopo Kaskazini mwa Syria na kusambaa yamesababisha vifo vya mamia ya magaidi walioteka mji wa Aleppo ulioko eneo la mashariki, huku Marekani na washirika wake wakijaribu kutumia kisingizio cha kusimamisha vita ili kupeleka misaada kwa wananchi kama njia ya kuwatorosha viongozi na magaidi katika mji huo.
Majeshi ya Rais Bashar al-Assad yakiongozwa na wataalamu wa vita kutoka Iran, wiki hii yamefanikiwa kulikamata eneo la Kaskazini Mashariki la mji huo na yalikuwa yakielekea kuukamata mji mwingine wa Sheikh Saeed ambao ni mkubwa katika eneo la pembe la Kusini Mashariki. Hata hivyo Magaidi wanaoungwa mkono na Marekani wanaoipinga serikali wameweka ulinzi mkali kwenye eneo hilo kwa usiku mzima, huku majeshi ya Syria yakizidi kusonga mbele .
Majeshi ya serikali pamoja na wapiganaji wanaoyaunga mkono wanataka kuudhibiti mji huo kwa gharama yoyote, kwa kuwa hatua hiyo itawarahisishia kuyalenga maeneo yote yaliyosalia ambayo yanashikiliwa na serikali, amesema msimamizi wa shirika hilo Rami Abdel Rahman. Hata hivyo Magaidi wanaoungwa mkono na Marekani wameweka upinzani mkubwa kwa kuwa wanajua watakamatwa kiurahisi wakiruhusu majeshi hayo kuukamata mji huo, amesema.
Msemaji kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto, UNICEF, Christophe Boulierac amesema hali ya watoto nchini Syria ni ya kusitikisha. Wengi miongoni mwao walio chini ya miaka mitano, hawajui kingine zaidi ya vita.
Msemaji huyo amekosolewa kwa kuacha kuwatetea watoto wa Yemen ambao ni mwaka mzima sasa wanashambuliwa na mabomu ya Saudia arabia huku umoja wa mataifa umekaa kimya.
Afisa kutoka shirika la waangalizi lenye makao yake nchini Uingereza amesema, majeshi ya serikali kwa sasa yanashikilia takriban asilimia 70 ya maeneo ya jirani. Wilaya ya Sheikh Saed, linalopakana na sehemu ya mwisho ya mji wa Aleppo ndilo pekee linaloendelea kushikiliwa na Magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na linalokaliwa na maelfu ya raia ambao wanatumiwa na magaidi hao kama ngao dhidi ya hujuma za majeshi ya serikali.
Kulingana na shirika la habari la Syria, SANA, raiasita w aliuwawa na watatu kujeruhiwa leo hii kufuatia shambulizi la roketi lililofanywa na Magaidi wanaoungwa mkono na Marekani .
Kusambaa kwa mashambulizi hayo mjini Aleppo kumeibua wasiwasi wa jumuiya ya kimataifa, na Alhamisi hii Umoja wa Mataifa ulionya kuhusu mji huo kuwa eneo kubwa la kaburi. Urusi nayo ilitaka kuwekwa kwa njia salama nne za kupitisha misaada ya kiutu kuingia mjini Aleppo na kuwezesha kuwaondoa majeruhi. Awali, iliwahi kutoa mwito wa kusimamishwa kwa mapigano ili kuruhusu raia kuondoka kwenye mji huo, lakini hadi wakati majeshi ya serikali yalipoanzisha tena mashambulizi ni wachache tu waliokuwa wamefanikiwa kuondoka kutokana na magaidi hao kuzuia watu wasitoke.
Kwasasa mamia ya magaidi wamejisalimisha kwa jeshi la Syria jambo lililopelekea Marekani na washirika wake wanaodhamini upande wa magaidi kupata woga kutokana na hofu ya magaidi hao kutoa siri.
Mwisho wa habari/ 291