Shirika la haari AhlulBayt 9a.s) ABNA: idadi hiyo ya wanajeshi 67 kutoka katika majeshi ya kivamizi ya Saudi Arabia na washirika wake, wamekipata kipigo hicho hata kufa baada ya shambulio maalumu la majeshi ya kujitolea wananchi wa Yemen katika sehemu hiyo.
Wizara ya ulinzi ya Yemen imetangaza kuwa: wanajeshi 67 kutoka katika jeshi la uvamizi wa Yemen chini ya usimamizi wa Saudi Arabia, walipata kipigo hicho baada ya kuingia katika mtego uliokuwa umetegwa na majeshi ya wananchi wa kujitoalea wa Yemen katika eneo la Nehim mashariki mwa Sana`a nchini Yemen.
Kamanda wa jeshi hilo la kivamizi la Saudi Araia aliyekuwa na jina la “ Jamil Muhammad Nasir” pia amekufa akiwa na wanajeshi weke wengine katika shambulio hilo.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Sabanet, ni kwamba: wavamizi wa Saudi Arabia wamepatwa na mstuko mkubwa baada ya kupata habari hiyo, na kuamua kukaa kimya na kuto tangaza kuhusu tukio hilo la kufa wanajeshi wake hao, huku habari zinasisitiza kuwa mpaka sasa vamilia za marehimu bado hazijjapiwa taarifa yeyote kuhusu ndugu zao.
mwisho/290
21 Desemba 2016 - 16:40
Msimbo wa Habari: 799822
Wanajeshi 67 kutoka katika majeshi ya kikosi cha (Al-Furqan) wameangamizwa na majeshi ya Yemen baada kuingia katika mtego uliotegwa na majeshi ya Yemen katika sehemu ya Nehim mashariki mwa mji mkuu wa Yemen Sana`a.