8 Januari 2017 - 14:23
 Watu 12 wafariki kufuatia mlipuko wa bomu Iraq

Watu 12 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa katika soko la mboga mashariki ya Baghdad, baada ya mlipuaji wa kujitoa muhanga...

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Watu 12 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa katika soko la mboga mashariki ya Baghdad, baada ya mlipuaji wa kujitoa muhanga, kuliripua gari alilokuwa ndani yake. Mlipuko huo umetokea katika wilaya ya Jamila ambayo inayokaliwa na waislamu wa dhehebu la shia. Maafisa wa polisi na wahudumu wa afya wamethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo. Msemaji wa wizara ya usalama Saad Maan amesema, mwanajeshi aliyekuwa kwenye lango la soko la Jamila, alimfyatulia risasi mlipuaji huyo punde alipotilia mashaka gari hilo, ndipo mlipuaji akalipua gari lake. Maan amesema mwanajeshi huyo ni miongoni mwa waliojeruhiwa. Kundi la kigaidi la waislamu wa dhehebu la Answari sunna au wahabia linalojiita Dola la Kiislamu au Daesh limedai kupitia mtandao kuwa ndilo limefanya shambulio hilo. Misururu ya mashambulio katika mji mkuu wa Iraq na miji mingine katika kipindi cha wiki moja, yamesababisha vifo vya watu kadhaa. Kundi hilo la kigaidi la Daesh lenye uhusiano wa karibu na Saudia arabia limedai kuhusika katika baadhi ya mashambulizi hayo.

Mwisho wa habari/ 291