Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, leo hii ametoa mwito kwa Rais wa Marekani Donald Trump wa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za urais ya kuuhamisha ubalozi wa Marekani nchini humo, uliopo Tel Aviv ambayo ni mji mkuu wa Israel na kuuepeleka mji mkuu wa Palestina Jerusalem. Netanyahu amesema baada ya kumaliza kikao chake cha wiki na baraza la mawaziri, kwamba ni lazima ubalozi wa Marekani uhamishiwe Jerusalem kwa kuwa huo ndio utakuwa mji mkuu wa Israel. Lakini pia Netanyahu amesema anaona kwamba ni wakati muafaka kwa balozi nyingine nyingi kuhamishiwa Jerusalem. hata hivyo, nia hiyo ya Trump itakuwa inapingana na msimamo wa muda mrefu wa Marekani wa kuuweka Ubalozi wake Tel Aviv.
Wapalestina, wamesisitiza kuwa Jerusalem mji wao mkuu wa Taifa lao, wakati Israel inadai mji huo wote kuwa ni makao makuu yake. Suala hilo limekuwa mwiba mkali katika mzozo uliodumu kwa miongo kadhaa kati ya Israel na Palestina.
Wapalestina wameapa kuulinda ardhi zao kwa nguvu zao zote na kwamba hawataruhusu Israel na washirka wake kudhulumu haki zao, Jamhuri ya kiislamu ya Iran ambayo ndio msaada mkubwa kwa wapalestina, imeahidi kuendelea kuwasaidia wapalestina kwa hali na mali.
Mwisho wa habari/ 291